Home Soka Rooney Kama Kawaida Yake

Rooney Kama Kawaida Yake

by Sports Leo
0 comments

Straika wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney ameonekana hadharani akiwa amelewa huku akiwa amezungukwa na wanawake katika klabu moja ya usiku huko jijini Vancouver  nchini Canada.

Rooney 33′ anakipiga katika klabu ya D.C United inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani na alisafiri na timu yake kwenda nchini Canada kupambana na Vancouver Whitecaps na baada ya mchezo huo ambao timu yake ilipoteza kwa bao 1-0 alionekana katika lifti ya jengo la hoteli akiwa na mwanamke ambaye hakutambulika.

Rooney akiwa na mke wake na watoto wao.

Kufuatia tukio hilo lililosambaa mitandaoni,Mke wa staa huyo Coleen Rooney 33′ alisafiri mpaka mjini Washington Dc ambapo inadaiwa anaweza kuharakisha uhamisho wa mmewe kurudi nchini Uingereza ambapo ilibidi ahamie mwezi january kwenda kuwa kocha mchezaji wa timu ya Derby country.

banner

Inadaiwa staa huyo alikula starehe kwa saa saba mfululizo na alitoka klabuni hapo saa kumi na moja alfajiri,Licha tukio hilo kumkera mke wake pia limesababisha mama huyo wa watoto wanne wa kiume kutembea mtaani bila kuvaa pete ya ndoa ya wawili hao walioanza mahusiano toka Colleen akiwa na miaka 12.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited