Site icon Sports Leo

Rudiger aiweka njia panda Chelsea

Mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger ameanza kuiweka mashakani klabu yake juu ya mustakabali wake mara baada ya kuanza kuhusishwa na vilabu vikubwa barani Ulaya kama Paris Saint German,Real Madrid na Bayern Munich.

Rudiger yupo ndani ya msimu wa mwisho darajani na mazungumzo ya mkataba mpya kati yake na waajiri wake hao.

Beki huyo amekuwa katika kiwango bora tangu kuajiriwa kwa kocha Thomas Tuchel katika viunga vya Stamford Bridge,kabla ya hapo alikuwa katika wakati mgumu chini ya Frank Lampard mpaka kuhusishwa na kuuzwa.

Chelsea sasa watapaswa kuongeza juhudi za kumshawishi beki huyo kubaki na inasemekana ni harakati za wakala wake katika kumtafutia mteja wake mkataba mnono kwani mkataba wake unaisha Juni 2022.

Exit mobile version