Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Saido Ntibazonkiza, ni mchezaji mzuri ila hawezi kukimbia kwasababu ya Umri wake ni mkubwa.
Manara amesema endapo Saido Ntibazonkiza angekua ni Mchezaji wa Simba angekua anacheza dakika 20 au 25 kutokana na umri wake tofauti na anavyotumika Yanga sc.
Msemaji huyo pia amesema umri wa Saido ni sawa na umri wake au Saido atakuwa na umri mkubwa kidogo kuliko yeye.
Pia alisisitiza kuwa winga mwenye kasi wa Yanga sc Tuisila ni mchezaji mzuri lakini ni mwana riadha hivyo sio aina ya wachezaji ambao Simba Sc inawahitaji.
Msemaji huyo wa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara aliongeza kuwa mchezaji pekee kutoka Yanga ambaye anaweza kucheza Simba ni Feisal Salum ” Fei Toto.