Home Soka ”Saido ni Mzee” Haji Manara

”Saido ni Mzee” Haji Manara

by Sports Leo
0 comments

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Saido Ntibazonkiza, ni mchezaji mzuri ila hawezi kukimbia kwasababu ya Umri wake ni mkubwa.
Manara amesema endapo Saido Ntibazonkiza angekua ni Mchezaji wa Simba angekua anacheza dakika 20 au 25 kutokana na umri wake tofauti na anavyotumika Yanga sc.
Msemaji huyo pia amesema umri wa Saido ni sawa na umri wake au Saido atakuwa na umri mkubwa kidogo kuliko yeye.
Pia alisisitiza  kuwa winga mwenye kasi wa Yanga sc Tuisila ni mchezaji mzuri lakini ni mwana riadha hivyo sio aina ya wachezaji ambao Simba Sc inawahitaji.
Msemaji huyo wa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara aliongeza kuwa mchezaji pekee kutoka Yanga ambaye anaweza kucheza Simba ni Feisal Salum ” Fei Toto.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited