Home Soka Samata Aweka Rekodi Wembley

Samata Aweka Rekodi Wembley

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Manchester City,Staa wa timu ya Aston Villa na Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika uwanja wa Wembley.

Uwanja huo unaomilikwa na chama cha soka nchini Uingereza(F.A) ambapo ulifanyika mchezo baina ya Aston Villa dhidi ya Manchester City mchezo wa fainali wa kombe la ligi ambapo Manchester City walishinda mabao 2-1 huku Samata akifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 41 baada ya city kutangulia kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 20′ na Rodri 30′.

Pia Samata aliyejiunga na timu hiyo akitokea Krc Genk ameweka rekodi nyingine ya kuwa mtanzania wa kwanza kufunga bao katika mchezo wa fainali uwanjani hapo na wiki kadhaa nyuma aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu nchini Uingereza.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited