Staa wa Taifa stars na klabu ya Krc Genk ya nchini Ubeligiji Mbwana Samatta amefunga pingu za maisha na mwanamke aitwaye Neima Mgange ndoa iliyofungwa usiku huu eneo la kijichi nyumbani kwa bibi harusi.
Shangwe na vigelegele vilitawala mtaani hapo baada ya taarifa za Samatta kufunga ndoa na mwanadada huyo kusambaa na umati wa watu kufurika kumuona staa huyo aliyeambatana na ndugu,jamaa na marafiki wakiwemo mastaa Himid Mao na Thomas Ulimwengu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.