Klabu za Man United na Borrussia Dortmund zimekubaliana kimsingi kuuziana mcheza Jadon Sancho kwa kiasi cha paundi 73M ambapo mchezaji huyo atajiunga na Man utd baada ya kukamilisha taratibu za kiafya.
Katika dili hilo klabu ya Man city itafaidika na mauzo ya mchezaji huyo kwa maana ndio klabu iliyomkuza katika akademi kabla ya kujiunga na Dortmund.
Kwa muda mrefu timu hizo zimekua na majadiliano kuhusu kuuziana mchezaji huyo lakini bei iliyowekwa na Dortmund ilikua kikwazo kwa Man united huku ikisemekana tayari mchezaji alishaonesha nia ya kujiunga na mashetani wekundu wakiwa tayari wameshakubalina mpaka maslahi binafsi huku akiwa na mkataba mfupi uliosalia klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.