Bingwa mtetezi wa Fainali ya Mataifa Afrika (Afcon) Timu ya Taifa ya Senegal imetinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Cameroon mabao 3-1 leo katika Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mchezo wa kundi C ya michuano hiyo.
Senegal imefuzu hatua hiyo ikiwa na pointi sita huku ikiwa imebakiza mechi moja tu dhidi ya Guinea ambayo itakuwa kibaruani dhidi ya Gambia saa 5:00 usiku kutafuta alama tatu ikiwa na alama moja baada ya sare dhidi ya Cameroon katika mchezo wa kwanza.
Katika mchezo huo Senegal inayonolewa na kocha mzawa Alliou Cisse ilifanikiwa kupata mabao yake kupitia Ismail Sarr dakika ya 16 huku Habib Diallo akifunga bao la pili dakika ya 71 na Sadio Mane alifunga bao la tatu dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Senegal inaungana na Cape Verde ambayo imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora ya kwenye fainali hizo zinazofanyika Ivory Coast, ikiwa ni mara ya pili kwenye historia yao.