Home Soka Serbia waiduwaza Ureno,Hispania yafuzu

Serbia waiduwaza Ureno,Hispania yafuzu

by Sports Leo
0 comments

Katika hali ya kushangaza timu ya Taifa ya soka ya Serbia imeiduwaza timu ya Taifa Ureno baada ya kuifunga kwa jumla ya mabao 2-1 mjini Lisbon na kufuzu michuano ya kombe la dunia Qatar 2022.

Ureno waliokuwa nyumbani licha ya wingi wa mashabiki wake hawakuweza kufua dafu licha ya kuhitaji alama moja tu kufuzu.

Renato Sanchez aliipatia goli la mapema Ureno dakika ya 2 tu ya mchezo na kuamsha matumaini makubwa ya kufuzu,kabla ya Dusan Tadic kuiswazishia Serbia dakika ya 33.Kipindi kilianza kwa Serbia waliokuwa wanazihitaji alama zote tatu kulishambulia sana goli la Ureno na wakati ambao watu wengi wakiamini mchezo huo ungekua sare na Ureno kujiandaa kushangilia ni mshambuliaji wa Fulham Mitrovi alipeleka kilio kwa Ureno baada kutupia goli la ushindi dakika ya 90.

banner

Serbia wamefanikiwa kumaliza kileleni wakiwa na alama 20 huku Ureno wakiwa na 17,mabingwa hao wa kombe la Ulaya 2016 wakiongozwa na nahodha wao Ronaldo watsubiri hatua za mtoano kuona kama watafuzu michuano hiyo mikubwa duniani.

Hispania wao wameungana na Ujerumani,Denmark,Ufaransa,na Serbia kufuzu baada ya kupata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Sweden ns kufuzu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited