SERGIO Ramos ambaye ni nahodha wa kikosi cha Real Madrid amecheza jumla ya michezo 606 akiwa ndani ya kikosi hicho tangu ajiunge kwenye kikosi hicho msimu wa mwaka 2005/06 na sasa ameomba kusepa kikosini hapo.
Ramos amewaeleza viongozi wa kikosi hicho kuwa amepata dili la maana kwenye moja ya timu nchini China hivyo hamna namna ya yeye kubaki kikosini hapo.
Imeelezwa kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kutoelewana na Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kutokana na lawama anazotupiwa kwamba anahusika kwenye kuboroga kwa kikosi hicho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.