Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limemfungia miezi sita na kumpiga faini ya Tsh. 500,000 Kocha wa timu ya Miembeni, Suleiman Mohamed kwa utovu wa nidhamu.
Kocha huyo alishangilia kwa kushusha suruali chini na kubaki na nguo ya ndani mbele ya mashabiki baada timu yake kushinda bao 1-0
Adhabu hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Kamati ya Mashindano ya ZFF, Hussein Ahmada, ni kwa mujibu kifungu namba 31 cha kanuni ya kuendesha mashindano hayo.
Hussein alisema Kocha huyo atatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya kipindi anachotumikia adhabu hiyo na akishindwa kulipa faini adhabu itaendelea mara mbili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Credit:Jami Forums