Home Soka Shikhalo Rasmi Kmc

Shikhalo Rasmi Kmc

by Dennis Msotwa
0 comments

Kipa Farouk Shikhalo ametua rasmi katika klabu ya Kmc baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Yanga sc ambako amedumu kwa misimu miwili alipojiunga akitokea Bandari Fc ya nchini Kenya.

Kipa ambaye bado ni kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga sc licha kutemwa kutokana na mapendekezo ya mwalimu Nasredine Nabi ametambulishwa rasmi na Kmc huku tayari akiwa amewasili katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu iliyopo Morogoro.

Hata hivyo Shikhalo anakabiliwa na ushindani mkubwa wa nafasi kikosini humo ambapo atachuana na mkongwe Juma Kaseja aliyejihakikishia nafasi katika milingoti ya klabu hiyo inayomilikiwa na manispaa ya Kinondoni.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited