Home Soka Simba Haoo Ubingwa

Simba Haoo Ubingwa

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mtanange uliopigwa uwanja wa Taifa.

Licha ya jitihada za wageni kutaka kumiliki mpira walijikuta wakifungwa bao la kwanza kwa shambulizi la kushtukiza na mpira kumkuta Hassan Dilunga aliyefunga bao dakika ya 8 ya mchezo huku beki wa Mwadui Augustino Samson akijifunga dakika ya 21 bao lililodumu mpaka dakika ya 57 ambapo nahodha John Boko aliongeza goli la tatu kwa kichwa na kufanya mpira kumalizika kwa mabao hayo.

Simba wamejikita kileleni kwa pointi 75 baada ya kucheza michezo 30 na mpaka sasa wana dalili zote za kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited