Klabu ya wanawake ya Simba queens imekamilisha usaijili wa mshambuliaji Aisha Juma ambaye msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa anakipiga ndani ya timu ya Alliance Girls ambapo amedumu kwa zaidi ya misimu miwili.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumika timu hiyo ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya wanawake kwa misimu miwili mfululizo sasa.
Msimu uliopita nyota huyo kwa mujibu wa rekodi za soka la wanawake mshambuliaji huyo machachari alitupia mabao 27.