Klabu ya Simba sc sasa imetangaza kuwa itautumia uwanja wa Jamhuri ulioko mkoani Morogoro kama uwanja wake wa nyumbani kutokana na uwanja wa Uhuru na Benjamini Mkapa kufungwa na Serikali kwa ajili ya kufanyiwa maboresho makubwa.
Awali Simba sc ilikua ikitumia uwanja wa Benjamini Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani lakini hivi sasa imelazimika kuhamia rasmi mkoani Morogoro kwa ajili ya michezo hiyo ambapo itacheza mechi dhidi ya Tanzania Priosons utakaofanyika Machi 06,Coastal Union (Machi 09),Singida Fountain Gate (Machi 12) na dhidi ya Mashujaa Fc (Machi 15).
Simba sc itautumia uwanja huo kwa ajili ya michuano hiyo ya ligi kuu ya Nbc lakini kwa ajili ya michuano ya kimataifa itautumia uwanja wa Benjamini Mkapa kutokana na Wizara husika kuruhusu michezo hiyo ya hatua ya makundi ya Caf na hatua ya mtoani kufanyika hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu nchini Simba sc ina alama 36 katika michezo 15 ya ligi kuu ya Nbc ikizidiwa na Azam Fc iliyoko nafasi ya pili ikiwa na alama 43 lakini imecheza michezo 19 ya ligi kuu na Yanga sc iliyo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 43 katika michezo 16 ya ligi kuu.