60
Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara (Vpl) namba (259) Simba sc dhidi ya Coastal Union uliopangwa kuchezwa Mei 11, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umeahirishwa, utapangiwa tarehe Nyingine ya kuchezwa (Kiporo).
Bodi ya ligi (TPLB) imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kutokana na changamoto za usafiri kwa Simba sc kuelekea mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Kaizer Chiefs.
Â
Simba sc inatakiwa kucheza na Kaizer Chief siku ya ijumaa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kisha kurudi nchini haraka kujiandaa na michezo inayofuatia.