Site icon Sports Leo

Simba Sc Waifuata Mashujaa Kigoma

Kikosi cha timu ya Simba sc kimewasili mkoani Kigoma kuivaa Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini utakaofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi saa kumi jioni.

Msafara wa kikosi hicho ambacho jana kilifanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la shirikisho nchini uliwasili katika uwanja wa ndege jijini Dar es salaam asubuhi ya leo ambapo sasa mchana tayari kikosi kimewasili salama mkoani humo.

Mastaa mbalimbali wakiwemo Saido Ntibanzokiza,Mohamed Hussein,Aishi Manula walikua ni sehemu ya msafara wa klabu hiyo uliowasili uwanja wa ndege Kigoma.

Mchezo huo utakofanyika jumamosi saa kumi jioni utakua wa ushindani kutokana kila timu kuhitaji alama tatu muhimu huku Simba sc ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 23 katika michezo kumi ya ligi kuu huku Mashujaa ikiwa na alama 9 katika michezo 12 nafasi ya pili kutoka mwishoni mwa msimamo.

Exit mobile version