Home Soka Simba sc Waingia Vunja Bei

Simba sc Waingia Vunja Bei

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa Klabu ya Simba leo Aprili 20, 2021 umeingia makubaliano ya kimkataba na mfanyabiashara maarufu Bongo, Fred Vunjabei kuuza jezi za klabu hiyo.        

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuendelea kutoa ajira kwa vijana kama ilivyokuwa sera ya aliyekua Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli pamoja na Rais Samia Suluhu anayeendeleza kuiongoza Tanzania baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki.

Barbara amesema kuwa wengi waliomba tenda kwa ajili kuingia makubaliano na Simba ila mwisho wa siku wamempata Mtanzania, Vunja Bei.

banner

Mkataba huo wa miaka miwili una Thamani ya kiasi cha Shilingi Bilioni mbili huku pamoja na jezi pia atatengeneza bidhaa nyingine za klabu hiyo kama tsherts,kofia,Bendera na kadhalika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited