Home Soka Simba SC watambulisha Mascot

Simba SC watambulisha Mascot

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya soka ya Simba imetambulisha mascot ambao watakuwa wakitumika katika michezo ya nyumbani kuleta hamasa na burudani kwa mashabiki wa timu hiyo watakaokuwa wakihudhuria michezo hiyo.

Simba imekuwa klabu ya kwanza nchini kutambulisha mascot kama zifanyavyo klabu mbalimbali duniani.

Mascot huwa ni watu maalumu ambao huvaa vinyago vinavyoendana na taswira au sura ya klabu husika.Klabu mbalimbali kubwa duniani zimekuwa na mascot kwa miaka mingi mfano Manchester United ya England yenye mascot maarufu ajulikanaye kama ‘Fred The Red’.

banner

Huu unatajwa kama ubunifu kwa Simba katika kuelekea tamasha la Simba day ambapo mascot hao watatambulishwa rasmi kwa wanachama,mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo yenye makao yake mtaa wa Msimbazi.

Simba SC kwasasa ipo katika wiki ya Simba ambapo shughuli mbalimbali zimeendelea kufanyika kuelekea kilele chake siku ya Jumapili tarehe 19 Septemba katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited