54
Daktari wa klabu ya Simba SC Tanzania Yassin Gembe, amesema wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba wasiwe na hofu kuhusu hali goli kipa wa klabu hiyo Aishi Manula, Gembe amesema Manula alipoteza fahamu jana baada ya gongana na mchezaji wa JKT Tanzania wakati anarukia mpira.
Daktari huyo anasema walimkimbiza hospitali ya kairuki na kupatiwa vipimo na matibabu na mpaka hivi sasa anaendelea vizuri.
“Napenda kuchukua nafasi kuwatoa hofu wapenzi na washabiki na Wanachama wa klabu ya simba kutokana na majeraha aliyopata golikipa wao Aishi Manula siku ya jana, mpaka ninapozungumza muda huu hali yake inazidi kuimarika vizuri’
Kilichotokea Uwanjani ni kwamba jana alipoteza fahamu baada ya kugongana na mchezaji wa timu ya JKT Tanzania wakati anarukia mpira, kwa hiyo tulimkimbiza Hospital ya Kairuki na tulipata huduma nzuri ambapo alifanyiwa vipimo vyote vinavyohitajika hivi ninavyozungumza Aishi Manula anaendelea vizuri kabisa tunasubiri tu uchunguzi wa mwisho wa madaktari bingwa na nina imani atapata ruhusa muda si mrefu, kwa hali hivi ilivyo tuzidi kumuombea dua na hapana shaka atakuwepo kwenye mchezo ujao.