Taarifa kutoka nchini Congo zinasema kuwa ofa ya Simba sc ya kuipata saini ya kinda wa Klabu ya DC Motemapembe Kareem Kamvuidi imekataliwa na klabu hiyo.
Simba imeonyesha nia ya kumuhitaji kiungo huyo lakini ofa ya Simba sc ya kwanza ilikuwa ni Mil.150 ambayo ilikataliwa kisha ikatumwa ofa ya pili ambayo ni Mil.230 nayo imetupiliwa mbali huku Klabu ya Dc MotemaPembe wakisema ofa wanayotaka wao ni Tsh. Bil.2.
Kutokana na dau hilo inawezekana Simba sc ikashindwa kumsajili kiungo huyo licha ya kumhitaji hasa ikizingatiwa ana umri mdogo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.