Home Soka Simba sc Yapaa,Morrison Abaki Dar

Simba sc Yapaa,Morrison Abaki Dar

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha Simba SCkimeondoka leo alfajiri  kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya wenyeji wao Kaizer Chiefs hapo siku ya Jumamosi Mei 15, 2021.
Akizungumza na Wanahabri Meneja wa klabu ya Simba Sc Patrick Rweyemamu amethibitisha kuwa kiungo wao mshambuliaji Bernard Morrison hajasafiri na timu hiyo kwenda Afrika Kusini kutokana na kutokamilisha baadhi ya mambo yake binafsi.
Patrick aliyerejeshwa Simba sc baada ya kutimuliwa akituhumiwa kuihujumu timu hiyo,ameongeza kuwa nyota huyo anatarajia kusafiri ili kuungana na timu hiyo Afrika Kusini pindi atakapokamilisha taratibu zote za safari.
Kikosi Kamili Kilichosafiri kuelekea Afrika ya Kusini ni kama ifuatavyo:
Makipa
Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim
Mabeki
Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na David Kameta.
Viungo
Jonas Mkude, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Francis Kahata na Taddeo Lwanga.
Washambuliaji
Medie Kagere, John Bocco, Ibrahim Ajib na Chris Mugalu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited