Site icon Sports Leo

Simba Sc yashusha kiungo fundi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba sc imemsajili kiungo mshambuliaji kutoka klabu ya Teungueth ya Senegal Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal.

Kiungo huyo alifanikiwa kucheza hatua za makundi za klabu bingwa Afrika akiwa na kikosi cha Teungueth amabyo iliingia makundi baada ya kuwashangaza Raja Casablanca katika hatua ya mtoani.

Katika michuano hiyo Sakho alicheza michezo 10 akifunga goli moja na akitoa pasi za usaidizi 2 na atajiunga mara moja na waajiri wake wapya huko Morocco walikoweka kambi.

Exit mobile version