Kocha mkuu wa timu ya Tanzania kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 Kim Poulsen ameeleza kuwa alipanga kuwaita wachezaji wa Yanga, Feisal Salum na Dickson Job kikosini kwake lakini imeshindikana kutokana na nyota hao kuwa na ratiba ngumu.
“Nilipanga kuwajumuisha Feisal na Job, lakini wanakabiliwa na mchezo wa fainali hivyo nimewaacha na nimechagua wengine ambao naamini wataiwakilisha nchi vyema,” amesema Kim.
Sambamba na hao kocha Kim alimhitaji kipa wa Mwadui Mussa Mbissa, kwenye kikosi chake lakini imeshindikana kutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa baadhi ya nyaraka zake za kusafiria ikiwemo ‘Visa’ hivyo kumuita Daniel Mgore wa Biashara United.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.