Site icon Sports Leo

Simba Sc,Yanga Sc Wapewa Vibonde

Klabu za Simba sc na Yanga sc zimepangiwa vibonde katika michuano ya kombe la Shirikisho nchini kutokana na droo iliyopangwa siku ya Novemba 29 mwaka huu iliyoshirikisha jumla ya timu 64 ikiwemo 16 za ligi kuu nchini.

Mabingwa watetezi Yanga sc watakutana na Hausung ya bingwa wa Ligi ya mkoa Njombe wakati Simba wakiwakaribisha Tembo FC Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tabora huku Azam wenyeji wa Alliance kutoka Mwanza.

Katika droo hiyo jumla ya timu 32 zitacheza kati ya Disemba 15 na 17 ambapo ratiba kamili itakua Singida Foutain Gate itaikaribisha Arusha City, KMC itacheza dhidi ACA Eagle,Dodoma Jiji watavaana na Magereza
FC huku JKT Tanzania watacheza dhidi ya Kurugenzi FC, Kagera Sugar wao watacheza dhidi ya Dar City, Geita Gold watavaana na Singida Cluster, Namungo watacheza dhidi ya Hollywood FC.

Tabora United watavaana na Monduli Coffee ya Arusha, Coastal Union watacheza dhidi ya Greenland FC, Ihefu watakuwa na Rospa FC, Tanzania Prisons dhidi ya TRA Kilimanjaro, Mtibwa Sugar dhidi ya Nyakagwe na Mashujaa FC dhidi ya Mbuga FC.

Exit mobile version