Klabu ya Simba sc imemvuta mshambuliaji Deo Kanda kutoka Tp mazembe ya Kongo kwa usajili wa mkopo wa msimu mmoja baada ya Pande mbili kukubaliana.
Taarifa iliyothibitishwa na Mabingwa hao mara tano barani Afrika imesema kuwa mshambuliaji huyo yupo nchini kwa lengo la kukubaliana maslahi binafsi na mabingwa hao mara mbili mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara na kisha kukamilisha taratibu za usajili.
Kanda 29′ ni mchezaji mzoefu wa soka la Afrika baada ya kuzitumikia timu za Dc Motema Pembe,As vita,Raja Casablanca na pia ameichezea timu ya taifa la Kongo mechi 21 akifunga magoli manne.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.