Kikosi cha klabu ya Simba sc kimewasili visiwani Zanzibar kushiriki katika michuano ya mapinduzi inayoendelea visiwani humo ambapo kikosi hicho kesho januari 8 kitavaana na Chipukizi Fc.
Kikosi hicho kiliwasili kwa boti na kupokelewa na mashabiki mbalimbali wa klabu hiyo ambao walikua na furaha hasa baada ya jana kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Wakati huo huo mshambuliaji Benard Morrison anaruhusiwa kucheza michuano hiyo licha ya kuzuiwa kucheza na Fifa mpaka hapo kesi yake ya msingi iliyofunguliwa na klabu ya Yanga sc katika mahakama ya usuluhishi masuala ya michezo Cas itakaposikilizwa rasmi kutokana na michuano hiyo kutotambuliwa na Caf na Fifa.