Home Soka Son ajitia kitanzi Spurs

Son ajitia kitanzi Spurs

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Mkorea Heung-Min Son ametia saini mkataba wa kuemdelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2026.

Son alijiunga na Spurs mwaka 2015 akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani,amesaini mkataba huo mara baada ya kushawishika na mradi wa kisoka wa timu hiyo na mkurugenzi wa klabu hiyo Fabio Paraticci.

Awali kulikuwa na hofu kwa mchezaji huyo kubaki hasa baada ya kuhusishwa kuondoka kwa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Harry Kane.

banner

Mchezaji huyo ameichezea Spurs michezo 197 ya ligi na kufunga magoli 70.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited