Site icon Sports Leo

Stamford Brigde Kupanuliwa

Serikali ya England imetoa kibali kwa klabu ya Chelsea kuendelea na mipango yake ya upanuaji wa uwanja wa Stamford Bridge ambao kwasasa unaingiza mashabiki 41,000 lakini ukipanuliwa unategemea kuingiza mashabiki 60,000.

Kibali hicho kimetolewa upya kwa Chelsea mara baada ya kibali kilichotolewa mara ya kwanza kuisha mwezi March-2020 lakini kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-19 imeifanya serikali kuongeza kibali hicho kwa mwaka mmoja mpaka mwezi Aprili-2021.

Klabu ya Chelsea ilipata kibali cha kufanya upanuaji wa uwanja huo mwezi March-2017 na ilitakiwa kidumu ndani ya miaka mitatu ambapo Chelsea ilitakiwa kuanza upanuaji ndani ya miaka hiyo mitatu.

Lakini kwasababu ambayo haikutajwa Chelsea iliandika walaka baadae ikitoa taarifa ya kusimamisha mipango yote ya upanuaji wa uwanja huo unaopatikana mitaa ya Fulham jijini London.

Lakini sababu iliyotajwa kufanya mipango hiyo kusimamishwa ni mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuishiwa na kibali chake cha kuishi nchini Uingereza.

Hivyo kibali hicho kilidumu kwa miaka mitatu mpaka mwishoni mwa mwezi March mwaka huu kilipoisha rasmi.

Lakini katikati ya mwezi March inajulikana kwamba ugonjwa wa Covid-19 uliishambulia dunia haswa nchini Uingereza na kusababisha shughuli zote kusimamishwa ikiwemo ligi kusimamishwa na hiyo kuwa sababu kwa Chelsea na serikali imesogeza mbele muda wa kibali hicho cha kuanza upanuaji kumalizika ambapo kwasasa kimesogewa mbele mpaka mwezi Aprili-2021 ambapo kwa mujibu wa taarifa bajeti nzima ya upanuaji huo wa kiwanja inatajwa kufikia paundi bilioni 1.

Viwanjani Leo

Exit mobile version