Mechi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia baina timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Madagascar inayotarajia kufanyika kesho Jumanne sasa utachezwa bila ya kuhudhuriwa na mashabiki wowote.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam mishale ya saa kumi na moja jioni.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Afisa habari wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF) Clifford Ndimbo katika mkutano na waandishi kuelekea mchezo huo wa pili kwa Stars katika kusaka tiketi ya kufuzu kombe ka dunia Qatar 2022,ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa juhudi za kupambana na ugonjwa wa Uviko-19 ambao ni janga la dunia.
Hilo ni pigo kwa kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen ambaye alikua anaamini kucheza nyumbani na mashabiki kungewaongezea hamasa na msukumo wachezaji wake katika kusaka pointi tatu muhimu wakiwa nyumbani hasa baada ya kuanza kwa sare katika mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo mjini Lubumbashi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo Stars imepata nguvu baada ya kurejea kwa nahodha wake Mbwana Samatta ambaye alikosekana katika mchezo wa kwanza alipokuwa akikamilisha maswala yake ya usajili kutua Royal Antwerp ya Ubelgiji.