Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” leo itajitupa tena uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani “Chan” katika michuano inayoendelea nchini Cameroon.
Stars inatakiwa ishinde mchezo huo ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu hatua inayofuatia huku ikijiwekea mazingira mazuri ndani ya kundi lenye timu za Guinnea,Namibia na Zambia.
Silaha pekee ya kutumainiwa ni uwepo wa mshambuliaji John Boko ambaye vyombo vya habari nchini Cameroon vimemtaja kama mtu wa kuchungwa katika mchezo huo utakaochezwa saa moja na nusu usiku kwa saa za kitanzania.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.