Home Soka Stars yapoteza nyumbani,Benin kinara kundi J

Stars yapoteza nyumbani,Benin kinara kundi J

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ mepoteza rasmi nafasi ya kufuzu hatua ya kumi bora Afrika kukata tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia mwakani katika nchi ya Qatar.

Hiyo ni baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 hii leo kwa DR Congo katika mchezo wake wa tano katika kundi J nyumbani katika ukanda wa Afrika licha ya kuwa na matumaini kibao ya kushinda mchezo huo kwa kufanya maandalizi ya kutosha.

Mabao ya DR Congo yamefungwa na Gael Kakuta,Nathan Fasika na Ben Malango na kushika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 8.

banner

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Benin wakiwa nyumbani wamepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Madagascar na kufikisha alama 10 kileleni mwa msimamo wa kundi hilo huku wakihitaji alama moja tu kwenye mchezo wa mwisho dhidim ya DR Congo ugenini kufuzu hatua inayofuata.

Stars imeshuka hadi nafasi ya tatu huku ikitarajiwa kumalizia mchezo wake wa mwisho tarehe 14 dhidi ya Madagascar ugenini katika mchezo usioamua chochote.

Msimamo kamili wa kundi hilo baada ya michezo ya leo

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited