Home Soka Stars,Madagascar Bila Mashabiki

Stars,Madagascar Bila Mashabiki

by Sports Leo
0 comments

Mchezo baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya timu ya Taifa ya Madagascar utakaofanyika kesho septemba 7 utachezwa bila mashabiki ikiwa ni tahadhari dhidi ya maambukizi ya Uviko 19 kwa mujibu wa shirikisho la soka barani Afrika (Caf).

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni huku Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika nchini Qatar 2022. Stars itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe.

Katika mchezo huo Stars inahitaji ushindi ili kujiweka sawa katika msimamo wa kundi lake ambapo ilifanikiwa kutoa sare dhidi ya Drc na sasa niz amu ya Magascar katika ardhi ya nyumbani tena ikiwa bila mashabiki.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited