Taarifa zinadai aliyekua kocha wa klabu ya Simba sc Sven Vandebroek ameishitaki klabu hiyo katika shirikisho la soka duniani(Fifa) baada ya kutomlipa baadhi ya stahiki zake ikiwemo bonasi za ushindi kwa mujibu wa mkataba wake.
Sven aliyeikacha Simba sc baada ya kufanikiwa kuivusha klabu hiyo amepeleka malalamiko hayo kufuatia kuahidiwa kulipwa mara kadhaa lakini haikua hivyo huku akidai baadhi ya fedha za mishahara pamoja na bonasi za ushindi wa taji la ligi kuu msimu wa 2019/2020.
Pia taarifa zinadai licha ya sababu hiyo pia kulikua na suala la kumpangia kikosi kwa viongozi kulazimisha Meddie Kagere aanze pamoja na mshambuliaji mwingine mfumo ambao kocha huyo hakuwa akiukubali hivyo kumlazimu kuachana na klabu hiyo.