Klabu ya Simba ipo mbioni kuachana na mastaa wasiopungua tisa katika kikosi cha sasa wakati wa dirisha dogo mwezi ujao.
Wachezaji hao watakaotemwa wengi wao itakua kwa kushindwa kuonyesha kiwango stahiki pamoja na kukosa nidhamu katika timu hiyo jambo ambalo uongozi umelikemea mara kwa mara.
Habari za ndani ya uongozi zinadai moja ya wachezaji waliokalia kuti kavu wamo Mbrazil Wilker Da Silva ambaye amekosa namba mbele nahodha John Boko na Meddie Kagere.
Habari za kuachwa kwa baadhi ya wachezaji zimeongelewa pia na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa ambaye alisema suala la kuachana na baadhi ya wachezaji na la muhimu na lazima.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Kuwaacha wachezaji ni suala linalotokea kwenye timu zote hivyo kwa sasa kunahitaji utulivu na umakini mkubwa ili kuwapata walio sahihi,” amesema Mazingisa.