Kiungo wa Simba Clatous Chama leo Jumatatu asubuhi Juni 8, ameanza mazoezi ya peke yake chini ya uangalizi wa Kocha wa Viungo, Adel Zrane baada ya kuchelewa kuanza na wenzake wiki mbili zilizopita.
Chama ambaye amerejea nchini jana kutoka nyumbani kwao Zambia, amechelewa kujiunga na wenzake kutokana na mipaka ya nchi hiyo kufungwa kutokana na mlipuko wa homa ya virusi vya corona.
Benchi la ufundi chini ya kocha, Sven Vandenbroeck limekuwa na utaratibu wa kuwapa mazoezi maalumu wachezaji wanaochelewa kuripoti mazoezini ili kuwaweka fiti kuendana na wenzake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Wiki iliyopita kiungo Francis Kahata naye alipewa mazoezi kama hayo baada ya kuchelewa kurejea kutoka Kenya sababu ikiwa ni ile ile ya mipaka kufungwa kutokana na corona.