Home Soka Torres wa city huyoo Barca

Torres wa city huyoo Barca

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na Manchester City kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Ferran Torres kwa ada ya paundi milioni 46.7 ambayo baadae itapanda hadi kufikia paundi milioni 55 kama nyongeza kutokana na kiwango atakachoonesha.

Mchezaji huyo kwasasa yupo nje ya uwanja kwa jeraha la mguu,ataiingizia City faida ya paundi milioni 27 kutokana na kununuliwa kwa kiasi cha paundi milioni 20 mwaka 2020 kutoka Valencia.

Barcelona inamtazama Torres kama mmoja ya vipaji vikubwa vinavyochipukia katika taifa la Hispania,na wamefanikiwa kumsajili kutokana na kupokea mkopo wa benki hivi karibuni.Lakini pia mahusiano yao na City ni mazuri kutokana na uwepo wa Txiki Begiristain na Ferran Soriano ambao waliwahi kufanya kazi na Rais wa sasa wa Barca Juan Laporta kipindi cha nyuma cha utawala wake.

banner

Torres mwenye umri wa miaka 21 amecheza michezo mine tu ya ligi kuu msimu huu akifunga magoli mawili na moja kwenye michuano ya kombe la la ligi ya mabingwa Ulaya.

Mchezaji huyo atasafiri hadi Hispania siku ya Ijumaa kufanyiwa vipimo vya afya,licha ya kusumbuliwa na majeraha ya mguu aliyopata alipokuwa akiitumikia timu ya taifa ya Hispania mwezi Oktoba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited