Home Soka Traore Aitosa Spain

Traore Aitosa Spain

by Sports Leo
0 comments

Winga wa Wolves Adamu Traore ameomba kujitoa kwenye kikosi cha Uhispania baada ya kupata jeraha siku moja tu baada ya jina lake kuitwa kikosi cha Uhispania mnamo Jumamosi.

“Kwa bahati mbaya, sitaweza kuhudhuria wito wa timu ya taifa kwa sababu ya jeraha nililopata mchezo dhidi ya Aston Villa jumapili, lakini nitaendelea kufanya jitihada na kujiweka fiti kwa kikosi kijacho, Mungu akipenda. Jumatatu hii nitakuwa nafanyiwa vipimo vya matibabu katika klabu yangu, ya Wolverhampton ili kujua kiwango cha jeraha nililonalo.” Traore alisema kwenye mtandao rasmi wa kijamii wa timu ya Uhispania.

Ikumbukwe kuwa Traore alichukua nafasi ya Rodrigo Moreno baada ya kukabiliwa na majeraha, sasa nafasi ya Adama itazibwa na Pablo Sarabia kutoka Paris St-Germain.

banner

Habari hii ni kwa mujibu wa Dominick Salamba.
.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited