Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limetoa viingilio vya mchezo wa ngao ya hisani baina ya Simba na Yanga unaotarajiwa kufanyika Septemba 25 katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Mchezo huo ni kuashiria ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 27 mwaka huu.
Kwa kawaida mechi ya ngao ya hisani husimamiwa na TFF tofauti na ligi kuu ambayo husimamiwa na bodi ya ligi,mechi hii huwakutanisha bingwa wa ligi kuu soka Bara na mshindi wa kombe la shirikisho la azam,na iwapo bingwa wa kombe la shirikisho ndiye bingwa wa ligi basi hukutana na mshindi wa pili kwenye msimamo wa ligi kuu.
Simba SC ndio mabingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho msimu wa 2020/2021,hivyo atakutano na Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili katika ligi katika mtanange mkali ukizingatia timu zote zimepoteza wikiendi iliyopita hivyo zitapambana kurejesha imani na furaha ya mashabiki wao
Viingilio hivyo ni kama inavyoonekana hapo chini: