Mahakama Kuu ya Tanzania imesitisha Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na kuwaita Rais wa TFF, Wallace Karia, Bodi ya Wadhamini & Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, kujibu hoja kwa nini uchaguzi huo usisimamishwe.
Wahusika hao Wametakiwa kufika mahakamani hapo leo asubuhi kujibu mashataka hayo na kama utetezi wao ukikosa mantiki mbele ya mahakama basi uchaguzi huo utasimamishwa.
Uchaguzi wa shirikisho la soka nchini uligumbikwa na malalamiko mengi kutoka kwa wagombea hasa baada ya kuwa na kipengele cha wadhamini ambacho wagombea wengi walishindwa kukidhi vigezo.