Timu ya Taifa ya Uingereza imefuzu kwenda robo fainali ya michuano ya euro baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Ujerumani kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mtoano uliofanyika katika la Wembley.
Uingereza ilijipatia bao la kwanza dakika ya 75 kupitia Raheem Sterling akipokea pasi ya Luke Shaw, na iliongeza bao la pili dakika ya 85 kupitia nahodha wake Harry Kane akimalizia kwa kichwa krosi ya Jack Grealish.
Hii ni mara ya kwanza kwa Uingereza kuifunga Ujerumani katika hatua za mtoano baada ya miaka 55.
Uingerza sasa itamsubiri mshindi kati ya Ukraine na Sweden katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayowashangaza wengi baada ya kuondolewa kwa vigogo watatu Ufaransa,Ureno na Ujerumani waliokuwa kundi moja.