Klabu ya Arsenal ya nchini England, imemtimua kazi kocha wake Unai Emery kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu hiyo kwenye mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu ya England pamoja na Europa League.
Unai anatemwa baada ya kuitumikia klabu hiyo takriban miezi 18 akiwa ameiongoza katika mechi 78, akishinda michezo 43, sare michezo 16 na kupoteza michezo 19.
Kwenye Ligi Kuu ya England ushindi wake ni asilimia 49 huku akiwa na rekodi mbaya zaidi klabuni hapo tangu mwaka 1992 ya kutoshinda mchezo wowote katika mechi saba mfululizo.
Unai raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 48, anatimuliwa ikiwa zimepita siku 54 tangu Arsenal ipate ushindi wake wa mwisho na asubuhi ya leo amehudhuria mazoezi ya timu kama kawaida bila kujua litakalomkuta.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Huyu ni kocha wa tatu kutimuliwa kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya Javi Garcia wa Watford na Mauricio Pochettino wa