Mkufunzi wa soka Luis Van Gaal amerejea tena kuifundisha timu ya taifa ya Uholanzi kwa mara ya tatu baada ya kile cha 2000-2002 na 2012-2014 katika michuano ya kombe la dunia.
Kocha huyo amechukua mikoba ya Frank De Boer aliyechemsha na timu hiyo kwenye michuano ya Euro 2020 na amekuwa bila ya kazi tyangu mwaka 2016 alipofukuzwa na Man Utd.
LVG amesema ‘ni heshima kurejea tena kuifundisha na Uholanzi,soka la Uholanzi siku zote limekuwa moyoni mwangu na timu ya Taifa ni ufunguo wa kulipeleka mbele soka letu’.
Van Gaal amepewa jukumu la kuipeleka Uholanzi kombe la dunia 2022 nchini Qatar pamoja na kuiongoza timu hiyo kwenye michuano hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.