Home Soka Wanyama Atua Marekani

Wanyama Atua Marekani

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa kimataifa wa Kenya Victor Wanyama amejiunga na klabu ya Montereal Impact iliyopo nchini Canada ambayo inashiriki ligi kuu ya Marekani(MLS).

Nahodha huyo wa Harambee Stars amejiunga na klabu hiyo ya nchini Canada iliyo ndani ya Major League Soccer kwa uhamisho huru na kusaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kumalizana na klabu ya Tottenham ya Uingereza .

Wanyama anaenda kunolewa na Straika wa zamani wa Arsenal na Barcelona  Thierry Henry ambaye ndie mkufunzi wa timu hiyo.

banner

Wanyama aliyezichezea timu za Celtic ya Skotland kisha akajiunga na Southampton ya Uingereza ambayo ilimuuza kwenda Tottenham.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited