Wakati timu ya Taifa ya Tanzania leo itatupa karata yake ya pili katika michuano ya mataifa ya Afrika kwawachezaji wa ndani maarufu kama Chan kikosi hicho kitawakosa mastaa watatu kutokana na majeraha.
Mastaa hao ni John Boko,Erasto Nyoni na Ibrahim Ame ambao bado hali zao za afya hajizatengemaa kisawa sawa kiasi cha kuhimili mikiki mikiki ya michuano hiyo.
Tegemeo pekee katika mchezo huo ni ushindi ili kusubiri matokeo ya michezo inayofuatia kuona kama Stars inaweza kupata nafasi baada ya kuruhusu kipigo cha mabao mawili kutoka kwa Zambia.