Home Soka Waziri atua Dodoma Jiji

Waziri atua Dodoma Jiji

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Mbao na Yanga Waziri Junior amejiunga rasmi na Dodoma Jiji kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwatumikia watoza ushuru hao wa makao makuu ya nchi.

Mchezaji huyo ametambulishwa rasmi muda mfupi uliopita kupitia ukurasa rasmi wa timu hiyo wa Instagram mchana huu.

Waziri aliachwa na mabingwa wa hkihistoria nchini Yanga baada ya kumalizika kwa msimu uliopita,ambapo baadae inasemekana alipta ofa kutoka moja ya vilabu vya Tunisia lakini dili hilo halikufanikiwa.

banner

Hivi karibuni aliipiga chini ofa ya Mtibwa sugar kutokana na sababu za kimaslahi pamoja na hali mbaya ya timu hiyo kwasasa kwenye msimamo wa ligi kuu soka ya NBC inayoendelea hapa nchini.

Kama atakuwa sawa kimwili huenda mchezaji akajumuishwa katika kikosi kitakachosafiri kuja Dar es salaam kukabiliana na waajiri wake wa zamani Yanga katika mchezo wa ligi utakaofanyika ijumaa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited