Home Soka Willian Achukua Nafasi ya Neymar Brazil

Willian Achukua Nafasi ya Neymar Brazil

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Bacchi maarufu kama Tite amemuita winga wa chelsea ya Uingereza Wilian kuchukua nafasi ya Neymar katika kikosi cha timu ya taifa hilo kinachojiandaa na michuano ya Kopa Amerika itakayofanyika nchini humo.

Tite amaefanya uteuzi huo baada ya nahodha wa zamani wa timu hiyo Neymar Jr kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya qatar wiki iliyopita.

Willian mwenye miaka 29 amechukua nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na benchi la ufundi la timu hiyo akimshinda kinda wa Real Madrid Vinicious Junior aliyekuwa akipewa kipaumbele na wadau wengi wa michezo duniani.

banner

Winga huyo mwenye kasi alicheza mechi yake ya mwisho mei 29 dhidi ya Arsenal ambapo aliwasaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited