Yanga ina kila sababu ya kufanya vizuri kwenye mechi zake baada ya GSM kuboresha mazingira ya wachezaji ikiwemo kuleta vitendea kazi vya kisasa
Siku za karibuni kwenye mazoezi ya Yanga baadhi ya wachezaji wanaonekana kuvaa vifaa maalum vya kupima ufanisi wao mazoezini ‘GPS vest.’
Vifaa hivyo ambavyo kocha aliyepita Mwinyi Zahera aliwahi kuvitaka, gharama yake ni Tsh Milioni 24 kwa kifaa kimoja.
Vinasaidia kufuatilia mwenendo wa mchezaji mmoja mmoja mazoezini na hata kwenye mechi pia zinahifadhi kumbukumbu muhimu kama umbali ambao mchezaji anakimbia, kupima mwendokasi n.k
Kutokana na gharama yake kuwa kubwa, ni timu chache barani Afrika ambazo huvitumia, vinatumika zaidi barani Ulaya na nchi zilizoendelea
Yanga inaweza kuwa klabu pekee ambayo inatumia vifaa hivyo hapa Tanzania na hata Afrika mashariki.