Site icon Sports Leo

Yanga sc Kukata Rufaa

Klabu ya Yanga sc inakusudia kukata rufaa kupiga adhabu aliyopewa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Fredrick Mwakalebela ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka mitano pamoja na faini ya shilingi milioni 7 za kitanzania.

Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Hassan Bumbuli alithibitisha kuhusu suala hilo ambapo wanasubiri nakala ya hukumu ili kukata rufaa.

“Tumechelewa kukata rufaa kwa kuwa tulikuwa tunasubiri muongozo wa TFF, lakini kama klabu hatujakubaliana na adhabu hiyo kwa makamu mwenyekiti wetu,” amesema Bumbuli.

Exit mobile version