Home Soka Yanga SC kuwafuata Rivers Alhamisi

Yanga SC kuwafuata Rivers Alhamisi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Yanga inatarajia kuondoka nchini siku Alhamisi kuwafuata wapinzani wao Rivers United ya Nigeria kwenye mchezo wa marejeano wa klabu bingwa Afrika hatua ya mtoano.

Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa goli moja bila na kujiweka katika mazingira magumu zaidi itakapokuwa ugenini mwishoni mwa wiki hii.

Mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Bwana Gumbo amesema kuwa timu ipo katika hali nzuri na wanaimani kuwa watapindua matokeo hayo ugenini.

banner

Gumbo ameelezea pia kuwa wataendelea kuwakosa wachezaji wake watatu wa kimataifa ambao ni Mayele,Aucho na Djuma Shabani kutokana na kuchelewa kwa ITC zao na pengine watajumuishwa kama Yanga watafanikiwa kufuzu hatua ya makundi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited